قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ ٱللَّهُمَّ رَبَّنَآ أَنزِلۡ عَلَيۡنَا مَآئِدَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ تَكُونُ لَنَا عِيدٗا لِّأَوَّلِنَا وَءَاخِرِنَا وَءَايَةٗ مِّنكَۖ وَٱرۡزُقۡنَا وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ ١١٤
Qāla 'īsabnu maryamallāhumma rabbanā anzil 'alaynā mā'idatam minas-samā'i takūnu lanā 'īdal li awwalinā wa ākhirinā wa āyatam minka warzuqnā wa anta khayrur-rāziqīn
Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku. 114
Maelezo ya chini
114 Isa akawaitikia, na akasema: Ewe Mola wetu Mlezi, uliye miliki mambo yetu yote! Tuteremshie chakula kutoka mbinguni, kiwe ni siku-kuu kwetu kitapo teremka kwa walio amini miongoni mwetu, kwa walio tangulia na walio taakhari, na kiwe ni muujiza wa kutilia nguvu wito wako, na uturuzuku riziki njema, na Wewe ndiye Mbora wa kuruzuku.