Surat Al-Ma'idah, aya 101

5:101

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَسۡـَٔلُواْ عَنۡ أَشۡيَآءَ إِن تُبۡدَ لَكُمۡ تَسُؤۡكُمۡ وَإِن تَسۡـَٔلُواْ عَنۡهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلۡقُرۡءَانُ تُبۡدَ لَكُمۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهَاۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ ١٠١

Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū lā tas'alū 'an ashyā'a in tubda lakum tasu'kum wa in tas'alū 'anhā hīna yunazzalul-qur'ānu tubda lakum 'afallāhu 'anhā wallāhu ghafūrun halīm

Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole. 101

Maelezo ya chini

101 Enyi mlio amini! Msimuulize Nabii mambo ambayo Mwenyezi Mungu amekuficheni mkataka yafichuliwe, na mkamuuliza Nabii katika uhai wake, kwani Qur'ani inamteremkia bado. Na Mwenyezi Mungu atakubainishieni itapo hitajika. Mwenyezi Mungu amekusameheni kwa yasiyo tajwa, hatokuadhibuni kwayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye wasaa katika upole. Basi hana papara katika kuadhibu.