Surat Al-Ma'idah, aya 100

5:100

قُل لَّا يَسۡتَوِي ٱلۡخَبِيثُ وَٱلطَّيِّبُ وَلَوۡ أَعۡجَبَكَ كَثۡرَةُ ٱلۡخَبِيثِۚ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ يَٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ١٠٠

Qul lā yastawil-khabīthu wat-tayyibu walaw a'jabaka kathratul-khabīthi fattaqullāha yā'ulil-albābi la'allakum tuflihūn

Sema: Haviwi sawa viovu na vyema ujapo kupendeza wingi wa viovu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, ili mpate kufanikiwa. 100

Maelezo ya chini

100 Ewe Nabii! Waambie watu: Si sawa sawa vile vizuri anavyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu na vibaya anavyo kuharimishieni. Kwani farka iliyo baina ya viwili hivyo kwa Mwenyezi Mungu ni kubwa, na hata hivyo vibaya vingawa ni vingi na vinawapendeza watu wengi. Basi enyi wenye akili! Ufanyeni ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu uwe ni kinga yenu isikupateni adhabu yake kwa kukhiari vilivyo vyema, na kujiepusha na viovu, ili mpate kuwa miongoni walio fuzu duniani na Akhera.