إِنَّا مَكَّنَّا لَهُۥ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَءَاتَيۡنَٰهُ مِن كُلِّ شَيۡءٖ سَبَبٗا ٨٤
Innā makkannā lahū fil-ardi wa ātaynāhu min kulli shay'in sababā
Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu. 84
Maelezo ya chini
84 Tumemtilia nguvu amri yake katika ardhi, akiendesha humo mambo kwa mazingatio yake na utawala wake. Na tukampa ujuzi mwingi kwa njia ambazo kwazo akiweza kuongoza mambo.