Surat Al-Kahf, aya 79

18:79

أَمَّا ٱلسَّفِينَةُ فَكَانَتۡ لِمَسَٰكِينَ يَعۡمَلُونَ فِي ٱلۡبَحۡرِ فَأَرَدتُّ أَنۡ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَآءَهُم مَّلِكٞ يَأۡخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصۡبٗا ٧٩

Ammas-safīnatu fakānat limasākīna ya'malūna fil-bahri fa arattu an a'ībahā wakāna warā'ahum malikun ya'khudhu kulla safīnatin ghasbā

Ama ile jahazi ilikuwa ya masikini za Mungu wafanyao kazi baharini. Nilitaka kuiharibu, kwani nyuma yao alikuwako mfalme anaghusubu majahazi yote. 79

Maelezo ya chini

79 Ama ile jahazi niliyo itoboa ilikuwa ni ya watu wanyonge wenye haja, ambao kazi yao ni ya baharini wakitafuta riziki yao. Basi mimi nikataka kukitia ila chombo chao kisitakikane. Kwani nyuma yao yuko mfalme mtindo wake ni kupokonya kila jahazi nzima. (Kughusubu, kupokonya, hata kukiitwa "kutaifisha" ni dhambi kubwa kabisa kwa Mwenyezi Mungu, kwani ni dhulma.)