Surat Al-Kahf, aya 74

18:74

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا لَقِيَا غُلَٰمٗا فَقَتَلَهُۥ قَالَ أَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا زَكِيَّةَۢ بِغَيۡرِ نَفۡسٖ لَّقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـٔٗا نُّكۡرٗا ٧٤

Fantalaqā hattā idhā laqiyā ghulāman faqatalahū qāla aqatalta nafsan zakiyyata bighayri nafsil laqad ji'ta shay'an nnukrā

Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuuwa. (Musa) akasema: Ala! Umemuuwa mtu asiye na kosa, na wala hakuuwa! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa! 74

Maelezo ya chini

74 Na baada ya kutoka kwenye jahazi ile wakaingia kuendelea na safari yao. Njiani wakamkuta kijana. Yule mja mwema akamuuwa yule kijana! Musa akasema kwa kuchukia: Unakwenda muuwa mtu asiye na kosa lolote, na wala hakumuuwa mtu yeyote? Hakika umefanya jambo ovu kweli kweli!