Surat Al-Kahf, aya 48

18:48

وَعُرِضُواْ عَلَىٰ رَبِّكَ صَفّٗا لَّقَدۡ جِئۡتُمُونَا كَمَا خَلَقۡنَٰكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةِۭۚ بَلۡ زَعَمۡتُمۡ أَلَّن نَّجۡعَلَ لَكُم مَّوۡعِدٗا ٤٨

Wa'uridū 'alā rabbika saffal laqad ji'tumūnā kamā khalaqnākum awwala marrati bal za'amtum allan naj'ala lakum maw'idā

Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutakuwekeeni miadi. 48

Maelezo ya chini

48 Na Siku hii watu watahudhurishwa kwa makundi wakipangwa kwa masafu kwa ajili ya hisabu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Tumekufufueni kutokana na mauti, kama tulivyo kuumbeni pale mara ya mwanzo. Na mmetujia peke yenu, mmoja, mmoja, bila ya mali, na bila ya wana. Na duniani mlikuwa mkikanusha kufufuliwa na kuhisabiwa.