وَكَذَٰلِكَ بَعَثۡنَٰهُمۡ لِيَتَسَآءَلُواْ بَيۡنَهُمۡۚ قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ كَمۡ لَبِثۡتُمۡۖ قَالُواْ لَبِثۡنَا يَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ يَوۡمٖۚ قَالُواْ رَبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا لَبِثۡتُمۡ فَٱبۡعَثُوٓاْ أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمۡ هَٰذِهِۦٓ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ فَلۡيَنظُرۡ أَيُّهَآ أَزۡكَىٰ طَعَامٗا فَلۡيَأۡتِكُم بِرِزۡقٖ مِّنۡهُ وَلۡيَتَلَطَّفۡ وَلَا يُشۡعِرَنَّ بِكُمۡ أَحَدًا ١٩
Wakadhālika ba'athnāhum liyatasā'alū baynahum qāla qā'ilum minhum kam labithtum qālū labithnā yawman aw ba'da yawmin qālū rabbukum a'lamu bimā labithtum fab'athū ahadakum biwariqikum hādhihī ilal-madīnati falyanzur ayyuhā azkā ta'āman falya'tikum birizqim minhu walyatalattaf walā yush'iranna bikum ahadā
Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi anajua zaidi muda mlio kaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa akuleteeni cha kukila. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala asikutajeni kabisa kwa yeyote. 19
Maelezo ya chini
19 Kama tulivyo walaza tuliwaamsha wapate kuulizana wenyewe kwa wenyewe wamelala muda gani? Mmoja wao akasema: Umekupitieni muda gani katika usingizi? Wakasema: Tumelala muda wa siku au baadhi ya siku. Walivyo kuwa hawana yakini nayo hayo wakasema: Mwachieni mambo haya Mwenyezi Mungu; kwani Yeye ni Mjuzi zaidi wa haya. Na ende mmoja wenu mjini, na achukue hizi sarafu za fedha achague chakula kizuri kabisa akuleteeni mle. Na awe na mafahamiano mema. Wala mambo yenu yasijuulikane na mtu yeyote.