وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَٱلسَّاعَةُ لَا رَيۡبَ فِيهَا قُلۡتُم مَّا نَدۡرِي مَا ٱلسَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنّٗا وَمَا نَحۡنُ بِمُسۡتَيۡقِنِينَ ٣٢
Wa idhā qīla inna wa'dallāhi haqqun was-sā'atu lā rayba fīhā qultum mā nadrī mas-sā'atu in nazunnu illā zannan wamā nahnu bimustayqinīn
Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Saa haina shaka, nyinyi mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini. 32
Maelezo ya chini
32 Enyi mnao kanya kufufuliwa! Akikwambieni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba agano la Mwenyezi Mungu la kuwalipa ni haki yenye kuthibiti, na Saa haina shaka itakuja, nyinyi mkisema: Sisi hatujui chochote khabari ya hiyo Saa ya Kiyama, wala ukweli wake; na sisi ni dhana ya kudhania tu kuwa hiyo Saa itakuja, wala hatuna yakini kuwa itatokea.