Surat Al-Jathiyah, aya 24

45:24

وَقَالُواْ مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنۡيَا نَمُوتُ وَنَحۡيَا وَمَا يُهۡلِكُنَآ إِلَّا ٱلدَّهۡرُۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِنۡ هُمۡ إِلَّا يَظُنُّونَ ٢٤

Waqālū mā hiya illā hayātunad-dunyā namūtu wanahyā wamā yuhlikunā illad-dahru wamā lahum bidhālika min 'ilmin in hum illā yazunnūn

Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipo kuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu. 24

Maelezo ya chini

24 Na walisema wenye kukanya kufufuliwa: Hapana uhai ila huu uhai wa duniani tu tulio nao sasa. Tunaishi na tunakufa. Na hapana nyuma ya hayo uhai baada ya kwisha kufa. Na hapana cha kututeketeza isipo kuwa kupita dahari, yaani zama na wakati. Wala wao hawasemi hayo kwa ujuzi na kuwa na yakini, bali ni kwa kudhania na kukisia tu.