قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرٗا ٩٦
Qul kafā billāhi shahīdā baynī wabaynakum innahū kāna bi'ibādihī khabīrā basīrā
Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona. 96
Maelezo ya chini
96 Sema: Kama mnaukataa Utume wangu, basi Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutuhukumu baina yangu na nyinyi, akathibitisha ukweli wa Ujumbe wangu kwenu. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kujua hali zenu, na Mwenye kuviona vitendo vyenu. Naye ni Mwenye kukulipeni kwa hivyo.