أَوۡ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٞ مِّن نَّخِيلٖ وَعِنَبٖ فَتُفَجِّرَ ٱلۡأَنۡهَٰرَ خِلَٰلَهَا تَفۡجِيرًا ٩١
Aw takūna laka jannatum min nakhīlin wa'inabin fatufajjiral-anhāra khilālahā tafjīrā
Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika. 91
Maelezo ya chini
91 Au uwe nacho kitalu Makka cha mitende na mizabibu chenye kupita mito kati yake! (Kwa kujua kuwa ardhi ya Makka ni kavu haioti kitu.)