Surat Al-Isra, aya 83

17:83

وَإِذَآ أَنۡعَمۡنَا عَلَى ٱلۡإِنسَٰنِ أَعۡرَضَ وَنَـَٔا بِجَانِبِهِۦ وَإِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ كَانَ يَـُٔوسٗا ٨٣

Wa idhā an'amnā 'alal-insāni a'rada wana'ā bijānibihī wa idhā massahush-sharru kāna ya'ūsā

Na mwanaadamu tunapo mneemesha hugeuka na kujitenga kando. Na inapo mgusa shari hukata tamaa. 83

Maelezo ya chini

83 Na hakika katika maumbile ya mwanaadamu ni kujidanganya na kukata tamaa. Tukimneemesha kwa kumpa uzima na ukunjufu wa mali, hupuuza kutukumbuka na kutuomba, na hujitenga nasi kwa kiburi na majivuno! Na akiguswa na shari, kama ugonjwa na ufakiri, huwa mwingi wa kukata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.