أَوۡ خَلۡقٗا مِّمَّا يَكۡبُرُ فِي صُدُورِكُمۡۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَاۖ قُلِ ٱلَّذِي فَطَرَكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٖۚ فَسَيُنۡغِضُونَ إِلَيۡكَ رُءُوسَهُمۡ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَۖ قُلۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبٗا ٥١
Aw khalqam mimmā yakburu fī sudūrikum fasayaqūlūna man yu'īdunā qulil-ladhī fatarakum awwala marratin fasayunghidūna ilayka ru'ūsahum wayaqūlūna matā huwa qul 'asā an yakūna qarībā
Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakaye turudisha tena? Sema: Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu! 51
Maelezo ya chini
51 Au umbo jingenelo lolote ambalo mnaona kwa mawazo yenu haliwezi kuwa hai, basi hapana shaka yoyote mtafufuliwa! Watasema kwa kuona ni muhali: Nani atakaye turejesha hivyo? Waambie: Atakurjesheeni Mwenyezi Mungu, yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza. Watakutikisia vichwa vyao kwa mastaajabu, nao wakisema kwa kejeli: Huko kufufuliwa unako tuahidi kutakuwa lini? Waambie: Nataraji kutakuwa karibu!