Surat Al-Isra, aya 40

17:40

أَفَأَصۡفَىٰكُمۡ رَبُّكُم بِٱلۡبَنِينَ وَٱتَّخَذَ مِنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنَٰثًاۚ إِنَّكُمۡ لَتَقُولُونَ قَوۡلًا عَظِيمٗا ٤٠

Afa'asfākum rabbukum bil-banīna wattakhadha minal-malā'ikati ināthan innakum lataqūlūna qawlan 'azīmā

Je! Mola wenu Mlezi amekuteulieni wavulana, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake? Kwa hakika nyinyi mnasema usemi mkubwa. 40

Maelezo ya chini

40 Subhanahu anayachukia wayasemayo makafiri kwamba Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Anasema: Mola wenu Mlezi amekufadhilisheni kuliko Mwenyewe kwa kukupeni nyinyi watoto wanaume wenye nguvu, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake kwa mnavyo dai? Kwa maneno yenu haya mnazua matusi makubwa.