وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ بِٱلۡعَهۡدِۖ إِنَّ ٱلۡعَهۡدَ كَانَ مَسۡـُٔولٗا ٣٤
Walā taqrabū mālal-yatīmi illā billatī hiya ahsanu hattā yablugha ashuddahū wa awfū bil-'ahdi innal-'ahda kāna mas'ūlā
Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa. 34
Maelezo ya chini
34 Wala msiyatumie mali ya yatima ila kwa njia iliyo bora kabisa, ya kuiamirisha na kuikuza. Na endeleeni hivyo mpaka huyo mtoto afike umri wa utambuzi kuweza kuendesha mambo yake. Na akisha fika hivyo basi mkabidhini mali yake, na timizeni ahadi zote mlizo chukua. Kwani Mwenyezi Mungu atamsaili (atamuliza) aliye vunja ahadi kwa kuvunja kwake, na atamhisabia kwa hayo.