قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ تَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَأَنتُمۡ شُهَدَآءُۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ ٩٩
Qul yā'ahlal-kitābi lima tasuddūna 'an sabīlillāhi man āmana tabghūnahā 'iwajan wa antum shuhadā'u wamallāhu bighāfilin 'ammā ta'malūn
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia aliye amini Njia ya Mwenyezi Mungu mkiitafutia kosa, na hali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. 99
Maelezo ya chini
99 Enyi Watu wa Kitabu! Vipi mnajaribu kumgeuza mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuifuata Haki aache Njia Iliyo Nyooka ya Mwenyezi Mungu wa Kweli, na mnajaribu kuikosoa Njia hiyo, na nyinyi mnajua kuwa hiyo ndiyo Haki? Wala Mwenyezi Mungu hakughafilika na vitendo vyenu, naye atakulipeni kwavyo.