قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعۡمَلُونَ ٩٨
Qul yā'ahlal-kitābi lima takfurūna bi'āyātillāhi wallāhu shahīdun 'alā mā ta'malūn
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha ishara za Mwenyezi Mungu, na ilhali kuwa Mwenyezi Mungu ni Shahidi kwa yote mnayo yatenda? 98
Maelezo ya chini
98 Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la amemuamrisha Mtume wake awahizi Watu wa Kitabu kwa kuendelea kwao kukufuru na kupotoka na kupotosha, akasema: Enyi Watu wa Kitabu! Huo ukafiri wenu hauna sura wala maana. Kwa sababu gani mnakanusha dalili, na hoja za Mwenyezi Mungu zenye kuthibitisha Unabii na Ukweli wa Muhammad? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvijua vitendo vyenu na atakulipeni malipo yake.