Surat Al-Imran, aya 92

3:92

لَن تَنَالُواْ ٱلۡبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ ٩٢

Lan tanālul-birra hattā tunfiqū mimmā tuhibbūna wamā tunfiqū min shay'in fa innallāha bihī 'alīm

KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua. 92

Maelezo ya chini

92 Enyi Waumini! Hamtoipata kheri kaamili mnayo itaka na itakayo mridhisha Mwenyezi Mungu ila mkitoa katika vitu mnavyo vipenda na mkatoa katika Sabili Llahi, Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa namna mbali mbali. Na chochote mnacho kitoa, kidogo na kikubwa, kilio bora au chenginecho, Mwenyezi Mungu anakijua. Kwani Yeye ni Mwenye Kujua, hapana kitu kilioko mbinguni au duniani kinacho fichikana naye.