كَيۡفَ يَهۡدِي ٱللَّهُ قَوۡمٗا كَفَرُواْ بَعۡدَ إِيمَٰنِهِمۡ وَشَهِدُوٓاْ أَنَّ ٱلرَّسُولَ حَقّٞ وَجَآءَهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ٨٦
Kayfa yahdillāhu qawman kafarū ba'da īmānihim washahidū annar-rasūla haqqun wajā'ahumul-bayyinātu wallāhu lā yahdil-qawmaz-zālimīn
Mwenyezi Mungu atawaongoaje watu walio kufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawafikia hoja zilizo wazi? Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. 86
Maelezo ya chini
86 Mwenyezi Mungu hakubaliani na watu walio kwisha shuhudia kuwa Mtume ni wa haki, na zikawajia dalili za kuonyesha hayo, kisha baada ya yote hayo wakamkataa, na wakakataa miujiza yake. Huo basi ni udhaalimu wao, na Mwenyezi Mungu hakubaliani na madhaalimu.