أَفَغَيۡرَ دِينِ ٱللَّهِ يَبۡغُونَ وَلَهُۥٓ أَسۡلَمَ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ طَوۡعٗا وَكَرۡهٗا وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُونَ ٨٣
Afaghayra dīnillāhi yabghūna walahū aslama man fis-samāwāti wal-ardi taw'an wakarhan wa ilayhi yurja'ūn
Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa? 83
Maelezo ya chini
83 Je, wanataka Dini isiyo kuwa Dini ya Muhammad, na hiyo ndiyo Dini ya Manabii wote? Dini hii ndiyo pekee Dini ya Mwenyezi Mungu anaye nyenyekewa na kila kilichomo mbinguni na duniani kwa ut'iifu, kwa kupenda na khiari, au kwa lazima kwa kufuata tabia na maumbile. Na kwake Yeye ndio viumbe vyote vinarejea.