هُوَ ٱلَّذِي يُصَوِّرُكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡحَامِ كَيۡفَ يَشَآءُۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ٦
Huwal-ladhī yusawwirukum fil-arhāmi kayfa yashā'u lā ilāha illā huwal-'azīzul-hakīm
Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo. Hapana Mungu ila Yeye, Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 6
Maelezo ya chini
6 Ni Yeye, Mwenyezi Mungu, ndiye anakuundeni, anakupeni sura na hali nyinyi mmo matumboni mwa mama zenu, kwa sura na umbo mbali mbali kama apendavyo Yeye. Hapana Mungu ila Yeye Mwenye nguvu katika ufalme wake, Mwenye hikima katika kuunda kwake.