Surat Al-Imran, aya 29

3:29

قُلۡ إِن تُخۡفُواْ مَا فِي صُدُورِكُمۡ أَوۡ تُبۡدُوهُ يَعۡلَمۡهُ ٱللَّهُۗ وَيَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ٢٩

Qul in tukhfū mā fī sudūrikum aw tubdūhu ya'lamhullāhu waya'lamu mā fis-samāwāti wamā fil-ardi wallāhu 'alā kulli shay'in qadīr

Sema: Mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyafichua Mwenyezi Mungu anayajua; na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. 29

Maelezo ya chini

29 Sema, ewe Nabii!: Mkiyaficha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha katika vitendo vyenu na kauli zenu ni sawa, kwani Mwenyezi Mungu anayajua yote, na anayajua yote yaliymo mbinguni na yaliyomo duniani, yanayo onekana na yanayo fichikana. Uwezo wake unapenya katika viumbe vyake vyote.