Surat Al-Imran, aya 24

3:24

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامٗا مَّعۡدُودَٰتٖۖ وَغَرَّهُمۡ فِي دِينِهِم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ ٢٤

Dhālika bi annahum qālū lan tamassanan-nāru illā ayyāmam ma'dūdātin wagharrahum fī dīnihim mā kānū yaftarūn

Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa Moto isipo kuwa kwa siku chache tu. Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe waliyo kuwa wakiyazua. 24

Maelezo ya chini

24 Hao wanao kataa miongoni mwa Mayahudi wamedanganyika kwa kukataa kwao na matumaini ya uwongo wanao jitamanisha nafsi zao ya kuwa Moto hautawagusa ila siku chache tu. Na kudanganyika huko na matamanio hayo yamewapelekea kuendelea kuzua katika dini yao kunako endelea.