Surat Al-Imran, aya 19

3:19

إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلۡإِسۡلَٰمُۗ وَمَا ٱخۡتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ ١٩

Innad-dīna 'indallāhil-islāmu wamakhtalafal-ladhīna ūtul-kitāba illā mim ba'di mā jā'ahumul-'ilmu baghyā baynahum waman yakfur bi'āyātillāhi fa innallāha sarī'ul-hisāb

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. 19

Maelezo ya chini

19 Hakika Dini ya Haki aliyo iridhi Mwenyezi Mungu ni Dini ya Tawhidi, ya Mungu Mmoja, na kumnyenyekea Yeye kwa usafi wa moyo. Mayahudi na Wakristo wamekhitalifiana na Dini hii, wakazua na wakabadilisha. Na wala kukhalifu kwao hakukuwa kwa kudanganyikiwa au kwa ujinga ilipo wajia ilimu, bali yalikuwa hayo kwa uhasidi na ushindani tu. Na mwenye kupinga Ishara za Mwenyezi Mungu, basi na angojee hisabu ya Mwenyezi Mungu, nayo yenda kasi mno.