شَهِدَ ٱللَّهُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَأُوْلُواْ ٱلۡعِلۡمِ قَآئِمَۢا بِٱلۡقِسۡطِۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ١٨
Shahidallāhu annahū lā ilāha illā huwa wal-malā'ikatu wa ulul-'ilmi qā'imā bil-qisti lā ilāha illā huwal-'azīzul-hakīm
Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 18
Maelezo ya chini
18 Mwenyezi Mungu amebainisha wazi katika maumbaji yake dalili na Ishara ambazo hawezi kuzipinga mwenye akili, ya kwamba Yeye ni Mmoja, wala hana mshirika wake, na kwamba Yeye ndiye Mwenye kusimamia mambo ya viumbe vyote kwa uadilifu. Na kwa haya pia wamekiri Malaika walio t'ahirika, na wameyajua watu wa ilimu kwa yakini, na kwamba Yeye ilio tukuka shani yake ni Mpweke katika Ungu, wala hana wa kumshinda katika jambo, na hikima yake imeenea kila kitu.