إِن يَنصُرۡكُمُ ٱللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمۡۖ وَإِن يَخۡذُلۡكُمۡ فَمَن ذَا ٱلَّذِي يَنصُرُكُم مِّنۢ بَعۡدِهِۦۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ١٦٠
In yansurkumullāhu falā ghāliba lakum wa in yakhdhulkum faman dhal-ladhī yansurukum mim ba'dihī wa'alallāhi falyatawakkalil-mu'minūn
Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. 160
Maelezo ya chini
160 Mwenyezi Mungu akikuungeni mkono kwa nusura yake, kama ilivyo tokea siku ya Badri, hatokushindeni yeyote. Na akikuacheni mkono kwa kuwa nyinyi hamkuchukua khatua zifaazo za ushindi, kama yaliyo pita siku ya Uhud, basi hamtakuwa na wa kukunusuruni mwenginewe. Na ni juu ya Mwenyezi Mungu peke yake ndio yawapasa Waumini wategemeze mambo yao yote.