وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّۚ وَمَن يَغۡلُلۡ يَأۡتِ بِمَا غَلَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ١٦١
Wamā kāna linabiyyin an yaghulla waman yaghlul ya'ti bimā ghalla yawmal-qiyāmati thumma tuwaffā kullu nafsim mā kasabat wahum lā yuzlamūn
Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana. Na atakaye fanya khiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa. 161
Maelezo ya chini
161 Haisihi kuwa Nabii yeyote kukhuni katika ngawira kama walivyo eneza kwa uzushi wanaafiki waongo. Kwani khiyana ni kinyume na Unabii. Basi isikupitikieni dhana hiyo. Na mwenye kukhuni atakuja Siku ya Kiyama na mzigo wa dhambi wa khiyana yake, tena kila nafsi italipwa ilicho tenda, kwa ukamilifu. Na wala hawatadhulumiwa kwa kupunguzwa thawabu zao wala kuzidishiwa adhabu yao.