Surat Al-Imran, aya 139

3:139

وَلَا تَهِنُواْ وَلَا تَحۡزَنُواْ وَأَنتُمُ ٱلۡأَعۡلَوۡنَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ١٣٩

Walā tahinū walā tahzanū wa antumul-a'lawna in kuntum mu'minīn

Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini. 139

Maelezo ya chini

139 Wala nyinyi msilegelege mkadhoofika katika Jihadi Fi Sabili Llahi kwa yanayo kupateni, na wala msihuzunike kwa wanao uliwa miongoni mwenu, kwani nyinyi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na Imani yenu na nguvu za Haki mnayo ipigania mko juu. Ushindi ni wenu ikiwa Imani yenu ni ya kweli, na maadamu mtadumu nayo.