Surat Al-Imran, aya 135

3:135

وَٱلَّذِينَ إِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةً أَوۡ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ ذَكَرُواْ ٱللَّهَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ لِذُنُوبِهِمۡ وَمَن يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ إِلَّا ٱللَّهُ وَلَمۡ يُصِرُّواْ عَلَىٰ مَا فَعَلُواْ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ ١٣٥

Walladhīna idhā fa'alū fāhishatan aw zalamū anfusahum dhakarullāha fastaghfarū lidhunūbihim waman yaghfirudh-dhunūba illallāhu walam yusirrū 'alā mā fa'alū wahum ya'lamūn

Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua. 135

Maelezo ya chini

135 Watu hao nao pindi wakifanya makosa makubwa au dhambi ndogo tu, mara humkumbuka Mwenyezi Mungu na Utukufu wake, na adhabu zake na malipo yake mema, na rehema yake na ghadhabu zake. Tena hapo hujuta kwa waliyo tenda na wakaomba msamaha wake, na hapana anaye samehe madhambi ila Mwenyezi Mungu. Na hao wachamngu hawabaki kuendelea juu ya jambo baya na ilhali wanajua ubaya wake.