Surat Al-Imran, aya 104

3:104

وَلۡتَكُن مِّنكُمۡ أُمَّةٞ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلۡخَيۡرِ وَيَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ ١٠٤

Waltakum minkum ummatun yad'ūna ilal-khayri waya'murūna bil-ma'rūfi wayanhawna 'anil-munkari wa ulā'ika humul-muflihūn

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa. 104

Maelezo ya chini

104 Hakika njia ya kuungana kuliko kamilika juu ya Haki katika kivuli cha Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kivuli cha Mtume wake, ni kuwa muwe nyinyi Umma unao lingania (unao itia) watu waje wafuate mwendo utao waletea maslaha ya Dini na dunia, uamrishe ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu, ukataze maasia. Na hapo ndipo mtakuwa mlio fuzu, kufuzu kulio kamilika.