Surat Al-Hashr, aya 14

59:14

لَا يُقَٰتِلُونَكُمۡ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرٗى مُّحَصَّنَةٍ أَوۡ مِن وَرَآءِ جُدُرِۭۚ بَأۡسُهُم بَيۡنَهُمۡ شَدِيدٞۚ تَحۡسَبُهُمۡ جَمِيعٗا وَقُلُوبُهُمۡ شَتَّىٰۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَعۡقِلُونَ ١٤

Lā yuqātilūnakum jamī'an illā fī quram muhassanatin aw min warā'i juduri ba suhum baynahum shadīdun tahsabuhum jamī'an waqulūbuhum shattā dhālika bi annahum qawmul lā ya'qilūn

Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili. 14

Maelezo ya chini

14 Mayahudi hawapigani vita nanyi kwa pamoja ila wawe katika miji iliyo jengewa ngome, au wajifiche nyuma ya kuta. Vita vyao baina ya wao kwa wao ni vikali. Utawadhani kuwa wameshikamana, wote ni wamoja. Kumbe hakika nyoyo zao zimefarikiana mbali mbali. Wao ni wenye sifa hizo, kwa sababu hao ni watu wasio zingatia nini utakuwa mwisho wa mambo.