Surat Al-Hashr, aya 13

59:13

لَأَنتُمۡ أَشَدُّ رَهۡبَةٗ فِي صُدُورِهِم مِّنَ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ ١٣

La antum ashaddu rahbatan fī sudūrihim minallāhi dhālika bi annahum qawmul lā yafqahūn

Hakika nyinyi ni kitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasio fahamu kitu. 13

Maelezo ya chini

13 Hakika, enyi Waislamu, mna kitisho zaidi katika vifua vya wanaafiki na Mayahudi kuliko wanavyo mwogopa Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa sababu hakika wao ni watu wasio jua ukweli wa Imani.