وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَلَا هُدٗى وَلَا كِتَٰبٖ مُّنِيرٖ ٨
Waminan-nāsi man yujādilu fillāhi bighayri 'ilmin walā hudan walā kitābim munīr
Na katika watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru. 8
Maelezo ya chini
8 Na juu ya yaliyo tangulia bado wapo baadhi ya watu wanao jadili juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu, na wanakanya kufufuka bila ya msingi wowote wa ki-ilimu, wala uwongozi wa kweli, au Kitabu kilicho toka kwa Mwenyezi Mungu cha kumwonyesha. Basi ubishi wake ni wa pumbao na inda tu.