وَكَأَيِّن مِّن قَرۡيَةٍ أَمۡلَيۡتُ لَهَا وَهِيَ ظَالِمَةٞ ثُمَّ أَخَذۡتُهَا وَإِلَيَّ ٱلۡمَصِيرُ ٤٨
Waka'ayyim min qaryatin amlaytu lahā wahiya zālimatun thumma akhadhtuhā wa ilayyal-masīr
Na miji mingapi niliipa muda na hali ilikuwa imedhulumu, na kisha nikaitia mkononi? Na kwangu Mimi ndio marudio yote. 48
Maelezo ya chini
48 Na wengi katika watu wa mijini walikuwa madhaalimu kama wao. Nami nikawapa muhula wala sikuwafanyia haraka kuwaadhibu. Na kisha nikawateremshia hiyo adhabu. Na ni kwangu Mimi tu ndio marejeo ya wote Siku ya Kiyama; na hapo nitawalipa kwa wanayo stahiki. Basi enyi makafiri! Msighurike kwa kuchelewa adhabu kukufikieni.