Surat Al-Hajj, aya 41

22:41

ٱلَّذِينَ إِن مَّكَّنَّٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَمَرُواْ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَنَهَوۡاْ عَنِ ٱلۡمُنكَرِۗ وَلِلَّهِ عَٰقِبَةُ ٱلۡأُمُورِ ٤١

Alladhīna im makkannāhum fil-ardi aqāmus-salawāta wa ātawuz-zakawāta wa amarū bil-ma'rūfi wanahaw 'anil-munkari walillāhi 'āqibatul-umūr

Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Swala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote. 41

Maelezo ya chini

41 Hao Waumini tulio waahidi kuwanusuru ndio hao ambao tukiwapa madaraka katika nchi wanalinda makhusiano yao na Mwenyezi Mungu na pia na wanaadamu wenzao. Kwa hivyo hushika Swala kwa utimilifu wake, na huwapa Zaka wanao stahiki kupewa, na huamrisha kila lenye kheri, na hukataza kila lenye shari. Na mambo yote hurejea kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Basi Yeye humtukuza amtakaye, na humdhalilisha amtakaye.