Surat Al-Furqan, aya 18

25:18

قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ مَا كَانَ يَنۢبَغِي لَنَآ أَن نَّتَّخِذَ مِن دُونِكَ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ وَلَٰكِن مَّتَّعۡتَهُمۡ وَءَابَآءَهُمۡ حَتَّىٰ نَسُواْ ٱلذِّكۡرَ وَكَانُواْ قَوۡمَۢا بُورٗا ١٨

Qālū subhānaka mā kāna yambaghī lanā an nattakhidha min dūnika min awliyā'a walākim matta'tahum wa ābā'ahum hattā nasudh-dhikra wakānū qawmā būrā

Watasema: Subhanak, Umetakasika na upungufu! Haikutupasia sisi kuchukulia walinzi badala yako, lakini Wewe uliwastarehesha wao na baba zao hata wakasahau kukumbuka, na wakawa watu walio angamia. 18

Maelezo ya chini

18 Jawabu yao itakuwa: Umetakasika, na Umetukuka! Haikutafalia sisi kabisa tumtake mlinzi badala yako atunusuru na aangalie mambo yetu. Basi itakuwaje juu ya haya tumtake yeyote atuabudu sisi badala yako Wewe? Lakini sababu ya ukafiri wao hawa ni kuwa uliwastarehesha kwa muda mrefu duniani, wao na baba zao. Hayo yakawapandisha kichwa, wakasahau kukushukuru, na kukuelekea Wewe tu kwa ibada. Basi wakawa kwa jeuri hiyo na ukafiri huo wanastahiki kuangamizwa.