وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ وَمَا يَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَقُولُ ءَأَنتُمۡ أَضۡلَلۡتُمۡ عِبَادِي هَٰٓؤُلَآءِ أَمۡ هُمۡ ضَلُّواْ ٱلسَّبِيلَ ١٧
Wayawma yahshuruhum wamā ya'budūna min dūnillāhi fayaqūlu a'antum adlaltum 'ibādī hā'ulā'i am hum dallus-sabīl
Na siku atakapo wakusanya wao na hao wanao waabudu, na akasema: Je! Ni nyinyi mlio wapoteza waja wangu hawa, au wao wenyewe walipotea njia? 17
Maelezo ya chini
17 Na taja, kwa ajili ya mawaidha, Siku ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya washirikina kwa ajili ya hisabu katika Siku ya Kiyama, pamoja na hao ambao walikuwa wakiwaabudu duniani badala ya Mwenyezi Mungu, kama Yesu (Isa), Ezra (Uzair) na Malaika. Mwenyezi Mungu atawauliza hao waabudiwa: Je! Ni nyinyi ndio mlio wapoteza waja wangu, mkawaamrisha wakuabuduni, au wao wenyewe ndio walio potea Njia kwa khiari yao, wakakuabuduni?