وَلَن يَتَمَنَّوۡهُ أَبَدَۢا بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّٰلِمِينَ ٩٥
Walan yatamannawhu abadā bimā qaddamat aydīhim wallāhu 'alīmu biz-zālimīn
Wala hawatayatamani kamwe kwa sababu ya yale yaliyo tangulizwa na mikono yao; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwajua vyema wanao dhulumu. 95
Maelezo ya chini
95 Lakini kwa hakika mambo yalivyo, wao hawayatamani mauti kabisa kwa dhulma walio ifanya, ambayo haifichikani kwa Mwenyezi Mungu. Yeye anawajua kuwa wao ni waongo kwa hayo wanao dai. Neema za Siku ya Kiyama zitakuwa ni za wachamngu, si za wafanyao maovu kama wao.