Surat Al-Baqarah, aya 94

2:94

قُلۡ إِن كَانَتۡ لَكُمُ ٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ عِندَ ٱللَّهِ خَالِصَةٗ مِّن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٩٤

Qul in kānat lakumud-dārul-ākhiratu 'indallāhi khālisatam min dūnin-nāsi fatamannawul-mawta in kuntum sādiqīn

Sema: Ikiwa nyumba ya Akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenu tu bila ya watu wengine, basi tamanini mauti kama nyinyi mnasema kweli. 94

Maelezo ya chini

94 Na nyinyi mmedai kuwa Mwenyezi Mungu atakupeni nyinyi tu neema za Pepo baada ya kufa, wasipate watu wote wengineo. Ikiwa basi kweli mnaamini hayo myasemayo basi yafaa myapende mauti. Hebu yatamanini myapate upesi zisije kutaakhari hizo starehe mnazodai.