Surat Al-Baqarah, aya 79

2:79

فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ يَكۡتُبُونَ ٱلۡكِتَٰبَ بِأَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ يَقُولُونَ هَٰذَا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ لِيَشۡتَرُواْ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلٗاۖ فَوَيۡلٞ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتۡ أَيۡدِيهِمۡ وَوَيۡلٞ لَّهُم مِّمَّا يَكۡسِبُونَ ٧٩

Fawaylul lilladhīna yaktubūnal-kitāba bi aydīhim thumma yaqūlūna hādhā min 'indillāhi liyashtarū bihī thamanan qalīlan fawaylul lahum mimmā katabat aydīhim wawaylul lahum mimmā yaksibūn

Basi ole wao wanao andika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyo andika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayo yachuma. 79

Maelezo ya chini

79 Basi hao makohani wataangamia na watapata adhabu kwa vile wanavyo andika vitabu kwa mikono yao, kisha wakawaambia wajinga wasiojua kusoma kuwa: Hii ni Taurati iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Kusudi lao ni kuwa wapate kwa hayo pato la upuuzi la kidunia, wanunue upuuzi huu kwa kuuza Haki na Kweli. Basi ole wao kwa wanayo mzulia Mwenyezi Mungu, na ole wao kwa yale matunda wanayo yachuma kwa uzushi wao!