وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ وَرَفَعۡنَا فَوۡقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ ٦٣
Wa idh akhadhnā mīthāqakum warafa'nā fawqakumut-tūra khudhū mā ātaynākum biquwwatin wadhkurū mā fīhi la'allakum tattaqūn
Na tulipo chukua ahadi yenu, na tukaunyanyua mlima juu yenu (tukakwambieni): Shikeni kwa nguvu haya tuliyo kupeni, na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kujilinda. 63
Maelezo ya chini
63 Kumbukeni pale tulipo chukua ahadi na agano juu yenu, tukaunyanyua mlima wa T'uur, tukaufanya kwa uwezo wetu kama kivuli juu yenu mpaka mkaogopa mkanyenyekea, tukakwambieni: Shikeni uwongofu na uwongozi tulio kupeni kwa nguvu na jitihadi, na mkumbuke kwa kutekeleza na kutenda yaliyo tajwa ndani ili mpate kujilinda nafsi zenu msipate adhabu.