وَإِن كَانَ ذُو عُسۡرَةٖ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيۡسَرَةٖۚ وَأَن تَصَدَّقُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ٢٨٠
Wa in kāna dhū 'usratin fanaziratun ilā maysaratin wa an tasaddaqū khayrul lakum in kuntum ta'lamūn
Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua. 280
Maelezo ya chini
280 Ikiwa mwenye kukopeshwa ana shida na uzito basi mpeni muhula wa kulipa deni lake mpaka wakati wa kufarijika. Na mkitoa sadaka kwa kusamehe deni au baadhi yake ni kheri yenu kama nyinyi ni watu wenye ujuzi na fahamu kuelewa maneno ya Mwenyezi Mungu anaye kufundisheni murwa na utu.