كَيۡفَ تَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَكُنتُمۡ أَمۡوَٰتٗا فَأَحۡيَٰكُمۡۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ٢٨
Kayfa takfurūna billāhi wakuntum amwātan fa ahyākum thumma yumītukum thumma yuhyīkum thumma ilayhi turja'ūn
Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akakufufueni! Kisha atakufisheni, tena atakufufueni, kisha kwake mtarejeshwa?. 28
Maelezo ya chini
28 Hakika hali yenu instaajabisha! Vipi mnakufuru na wala hapana sababu yoyote ya kutegemewa katika kukufuru kwenu? Ukiangalia hali yenu utaona inakataa ukafiri huu wala hamna udhuru wowote. Kwani nyinyi mlikuwa maiti, hamna uhai, akakuumbeni Mwenyezi Mungu na akakupeni uhai na umbo zuri. Kisha ni Yeye atakaye kurejezeni muwe maiti baada ya kutimia wakati wenu. Kisha atakufufueni muwe hai mara nyingine kwa ajili ya hisabu na malipo. Kisha mtarejea kwake, wala hamwendi kwa mwenginewe, mtarejea, kwa ajili ya hisabu na malipwa kwa vitendo vyenu.