ٱلشَّيۡطَٰنُ يَعِدُكُمُ ٱلۡفَقۡرَ وَيَأۡمُرُكُم بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ وَٱللَّهُ يَعِدُكُم مَّغۡفِرَةٗ مِّنۡهُ وَفَضۡلٗاۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ ٢٦٨
Ash-shaytānu ya'idukumul-faqra waya'murukum bil-fahshā'i wallāhu ya'idukum maghfiratam minhu wafadlan wallāhu wāsi'un 'alīm
Shet'ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua. 268
Maelezo ya chini
268 Shetani anakutieni khofu kuwa mtafakirika kwa kutoa, na kazi yake kutia ila kila kitendo chema, ili msitoe kwa ajili ya mambo ya kheri na mghurike na maasi. Na Mwenyezi Mungu aliye Mkunjufu wa kusamehe, ni Muweza wa kukutoshelezeni. Hapana lolote katika mambo yenu linalo fichikana kwake.