Surat Al-Baqarah, aya 263

2:263

۞ قَوۡلٞ مَّعۡرُوفٞ وَمَغۡفِرَةٌ خَيۡرٞ مِّن صَدَقَةٖ يَتۡبَعُهَآ أَذٗىۗ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَلِيمٞ ٢٦٣

Qawlum ma'rūfun wamaghfiratun khayrum min sadaqatin yatba'uhā adhan wallāhu ghaniyyun halīm

Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole. 263

Maelezo ya chini

263 Kauli ya kupoza nyoyo na ya kumsitiri hali fakiri usimwambie mwenginewe ni bora kuliko kumpa na baadae ukafuatizia maudhi kwa maneno au vitendo. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la si mwenye kuhitaji watu watoe na huku wanawaudhi mafakiri. Na Yeye anawawezesha mafakiri kupata riziki njema. Wala hafanyi haraka kumuadhibu asiye toa kwa matarajio huenda akaongoka akatoa.