يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُبۡطِلُواْ صَدَقَٰتِكُم بِٱلۡمَنِّ وَٱلۡأَذَىٰ كَٱلَّذِي يُنفِقُ مَالَهُۥ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۖ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ صَفۡوَانٍ عَلَيۡهِ تُرَابٞ فَأَصَابَهُۥ وَابِلٞ فَتَرَكَهُۥ صَلۡدٗاۖ لَّا يَقۡدِرُونَ عَلَىٰ شَيۡءٖ مِّمَّا كَسَبُواْۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ ٢٦٤
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū lā tubtilū sadaqātikum bil-manni wal-adhā kalladhī yunfiqu mālahū ri'ā'an-nāsi walā yu'minu billāhi wal-yawmil-ākhiri famathaluhū kamathali safwānin 'alayhi turābun fa asābahū wābilun fatarakahū saldal lā yaqdirūna 'alā shay'im mimmā kasabū wallāhu lā yahdil-qawmal-kāfirīn
Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri. 264
Maelezo ya chini
264 Enyi Waumini! Msipoteze thawabu za sadaka zenu kwa kudhihirisha kuwa mnawafadhili wenye haja na kuwaudhi. Hivyo mnakuwa kama wale wanao toa mali zao kwa ajili ya kutafuta umaarufu na kupenda wasifiwe na watu., nao hata hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Hali ya mwenye kuonyesha kutoa kwake ni hali ya jiwe manga lenye udongo. Likateremkiwa na mvua kubwa, udongo wote ukaondoka. Basi kama mvua kubwa inavyo chukua udongo wenye mbolea likabaki jiwe tupu, basi kadhaalika masimbulizi, na maudhi, na kuonyesha watu huharibu thawabu za sadaka. Hayo hayamnufaishi mtu, na hizo ni sifa za makafiri. Epukaneni nazo! Kwani Mwenyezi Mungu hawawafikishi makafiri kupata kheri na uwongozi mwema.