Surat Al-Baqarah, aya 257

2:257

ٱللَّهُ وَلِيُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّٰغُوتُ يُخۡرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَٰتِۗ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ٢٥٧

Allāhu waliyyul-ladhīna āmanū yukhrijuhum minaz-zulumāti ilan-nūri walladhīna kafarū awliyā'uhumut-tāghūtu yukhrijūnahum minan-nūri ilaz-zulumāti ulā'ika ashābun-nāri hum fīhā khālidūn

Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu. 257

Maelezo ya chini

257 Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuyaangalia mambo ya Waumini, na ndiye Mwenye kuwasaidia na kuwanusuru. Huwatoa kwenye kiza cha shaka na kudanganyikiwa kuendea kwenye nuru ya Haki na utulivu. Na Makafiri wenye kumkanya Mwenyezi Mungu wanashughulikiwa na Mashetani na wanao lingania shari na upotovu. Wao hao huwatoa kwenye nuru ya Imani walio umbiwa nayo na iliyo zagaa kwa dalili nyingi na ishara, na kuwatia kwenye kiza cha ukafiri na ufisadi. Na hawa makafiri ndio watu wa Motoni, na humo watadumu milele.