۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ خَرَجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَهُمۡ أُلُوفٌ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِ فَقَالَ لَهُمُ ٱللَّهُ مُوتُواْ ثُمَّ أَحۡيَٰهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ ٢٤٣
Alam tara ilal-ladhīna kharajū min diyārihim wahum ulūfun hadharal-mawti faqāla lahumullāhu mūtū thumma ahyāhum innallāha ladhū fadlin 'alan-nāsi walākinna aktharan-nāsi lā yashkurūn
Hukuwaona wale walio toka majumbani kwao kwa maelfu kwa kuogopa mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha akawahauisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru. 243
Maelezo ya chini
243 Zingatia, ewe Nabii, hichi kisa cha ajabu, na ukijue! Hao watu walitoka wakaacha majumba yao ati wanakimbia Jihadi kwa kuogopa kufa, na hali wao ni maelfu kwa maelfu. Mwenyezi Mungu akawahukumia kifo na udhalili kutokana na maadui zao. Walipo bakia walio bakia wakasimama kupigana Jihadi, Mwenyezi Mungu aliwapa uhai kwa kuwapa nguvu. Hakika uhai huu wenye nguvu ulio kuwa baada ya madhila umekuja kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, na unastahiki shukrani. Lakini wengi wa watu hawashukuru.