Surat Al-Baqarah, aya 225

2:225

لَّا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغۡوِ فِيٓ أَيۡمَٰنِكُمۡ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتۡ قُلُوبُكُمۡۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ ٢٢٥

Llā yu'ākhidhukumullāhu bil-laghwi fī aymānikum walākin yu'ākhidhukum bimā kasabat qulūbukum wallāhu ghafūrun halīm

Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi. Bali anakushikeni kwa yanayo chuma nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole. 225

Maelezo ya chini

225 Mwenyezi Mungu amekusameheni baadhi ya yamini (viapo) zenu. Lilio mpitia mtu ulimini mwake katika viapo bila ya kukusudia wala kulitia moyoni, au akaapa kwa kuamini kuwa limetukia na halikutukia, Mwenyezi Mungu hayachukulii hayo. Lakini anakushikeni kwa mnayo yaazimia katika nyoyo zenu kuwa yamekuwa au hayakuwa, na kwa kusema uwongo pamoja na kuuwapia yamini. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumghufiria mwenye kutubu, ni Mpole, anasamehe lisilo kusudiwa moyoni.